Saturday, February 1, 2014

DAWA YA KUZUIYA CHUMAULETE KATIKA BIASHARA


Kama unasumbuliwa na tatizo la kupoteza hela katika biashara katika hali isiyo ya kawaida. Unaweza ukafanya biashara yako vizuri lakini hela ukawa hauiyoni, fanaya mambo yafuatayo;

Chukua habbati soda iliyo sangwa vijiko 3 changanya na miski ya unga nusu ya kijiko. Toneshea matone ya mafuta ya sidiri huku ukiupuchua kwa mikono huo mchanganyiko wako wa dawa mpaka uhakikishe mchanganyiko wako wote uwe umeenea mafuta ya sidiri. Zingatia kuwa mchanganyiko wako inatakiwa uwe umeenea mafuta ya sidiri lakini uwe katika hali ya ukavu (vumbi)

Uweke mchanganyiko wako huo katika  chupa ndogo ya kioo, funga mdomo wa chupa kisha livishe chupa lako kitambaa chenye rangi ya weusi au rangi nyekundu. Kalichimbie chupa lako na ulifukie sehemu ambayo kiasili hua haiyoti mimea au jaani (jalala la taka) au chini ya jiko la mafiga ya kuni, wakati wa usiku, liache hapo kwa muda wa siku saba kisha ulitoe na ulivue kitambaa, muda wa kulitoa ni lazima iwe mchana wakati jua lipo katikati ya dunia

Tumia dawa yako hiyo kwa kuirashia takita droo yako ya hela au sehemu unayo weka hela fanya zoezi hilo kila baada ya siku 7. Itunze dawa yako katiaka sehemu nzuri, epuka sehemu ambayo mwanamke anaweza akaishika akiwa katika hali ya hedhi.

Dawa hii inanguvu za ajabu za kuzuiya aina zote za chuma ulete.

Tafadhali usisome kisha ukaondoka bila ya kuacha maoni yako  au ushauri. Mualike na mwenzio ajitibu kipitia blog hii.

4 comments:

  1. thats haraam brother if you r really muslim.... sio tiba sahihi,its shirki. muogope mungu wko

    ReplyDelete
  2. Dr kanyat mtaalamu wa tiba asili pia ni mganga wa jadi toka tanga ..anatibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia mizizi .mitishamba na dawa za kisuna ..anatibu nguvu za kiume ..uzazi ..ugumba ..kuzibua mirija ..maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.....miguu kuwaka moto..kurefusha na kunenepesha uume ..kubana uke uliopwaya ..mikosi..majini...wasiliana nae kupitia 0764839091

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kutufahamisha dawa nzuri ya chuma ulete

    ReplyDelete