Saturday, February 8, 2014

DAWA YA MAJERAHA NA VIDONDA SUGU


Tibu jeraha haraka na ondoa kovu sehemu hiyo ya jeraha kwa kufuata hatua zifuatazo;
Changanya na usage dhafarani ya unga na kaafuri kiasi cha kidonge kimoja cha kaafuri kwa vijiko viwili vya dhafarani

Weka maji jikoni yaache yachemke vizuri kisha yatowe jikoni hali ya kuwa umeyafunika yaache yapowe mpaka yawe vuguvugu. Osha sehemu yenye jeraha kwa maji hayo vuguvugu kisha weka kwa kunyunyiza kidogokidogo huo mchanganyiko wako wa kaafuri na dhafarani

Hakikisha kuwa umeweka sehemu yote ya donda, subiri kwa muda kidogo mpaka majimaji yakauke katika hilo jeraha kisha pakaa Asali mbichi sehemu ya juu ya jeraha lote, usilifunge jeraha lako liache wazi liwe linapitiwa na upepo, (Muhimu jeraha haliwezi kuadhiriwa na vijidudu likiwa limewekwa Asali,)

Fanya zoezi hilo asubuhi na jioni mpaka sehemu ya juu ya jeraha ifunge kwa kiwambo(ngozi laini yenye rangi nyekundu) hapo utaacha kutumia mchanganyiko wa kaafuri na asali, utakua unaosha kisha unapakaa maji ya Mti wa Aloe vera, unaacha kwa muda mpaka yakauke kisha unapakaa asali.

Endelea na zoezi hilo mpaka itakaporejea ngozi yako ya asili. Utarajibu huu wa tiba ya majeraha unatibu majeraha hata yale yaliyoisha sumbua kwa muda mrefu. Tiba hii hutibu majeraha ya aina zote.

Tafadhali usiondoke bila kuacha maoni yako na ushauri kwa ku comment hapo chini.




Tuesday, February 4, 2014

DAWA YA KUBATILISHA NZYONGO

Nzyongo ni aina ya uchawi unaotumiwa kuwadhuru watu kupitia macho,upepo na maji
kama umedhuriwa na nzyongo chukua majivu changanya na maji kisha jipakae mwili mzima zyomgo litaondoka  mara nyingi zyongo ni michezo midogo midogo ya kichawi ikiwa halitoondoka basi litakua ni tatizo lingine.

Saturday, February 1, 2014

DAWA YA KUMFUKUZA JINI/SHETANI KATIAKA ENEO LAKO LA BIASHARA


Ukitaka kumfukuza jini katiaka eneo la biashara zako;1 Chukua mafuta ya kitunguu swaumu,2 mafuta ya karafuu kali,3 mafuta ya mnyonyo, 4 mafuta ya sidiri, 5 mafuta ya kasa (aina ya samaki mwenye kijungu cha mafuta), 6 mafuta ya zaituni, 7 mafuta ya habati soda yote kiasi cha robo lita

Yamimine mafuta yote hayo katiaka chungu, kisha changanya na dawa zifuatazo; 1 karafuu maiti 2 mvuje 3 miati saila 4 misk ya  unga nyeusi 5 ambari 6 Unga wa mifupa ya samaki 7 mwanga jini

changanya vizuri dawa hizo katika hicho chungu cha mafuta kwa kukoroga

Weka jiko katiaka eneo lako la biashara, chemsha chungu hicho kikiwa wazi, acha kiendelee kuchemka kwa muda wa masaa 24 kwa siku ya kwanza, siku ya pili utachemsha kwa muda wa lisaa limoja kwa kuanzia saa ulio tolea kwa siku ya kwanza. Mfano; siku ya kwanza kama ulichemsha kwa kuanzia saa 1:00 asubuhi, utaitoa siku ya pili saa 1:00 asubuhi, siku hiyo ya pili utaiyacha, siku ya tatu utaichemsha kuanzia saa 1:00 hadi saa 2:00 siku ya tatu utaanzia saa 2:00 hadi saa 3:00 na utendelea na utaratibu huo kwa muda wa siku 7

Ukimaliza chungu hicho kakichimbie chini porini. tafadhali saana usikitupe hicho chungu sehemu yoyote,
Ukifanya kwa utaratibu huo jini ataondoka na kukimbia eneo hilo na hato rudi tena.

Tafadhali tunakuomba usiondoke bila kuacha maoni yako na ushsuri. pia mualike mwenzio ajitibu kupitia blog hii 


DAWA YA KUZUIYA CHUMAULETE KATIKA BIASHARA


Kama unasumbuliwa na tatizo la kupoteza hela katika biashara katika hali isiyo ya kawaida. Unaweza ukafanya biashara yako vizuri lakini hela ukawa hauiyoni, fanaya mambo yafuatayo;

Chukua habbati soda iliyo sangwa vijiko 3 changanya na miski ya unga nusu ya kijiko. Toneshea matone ya mafuta ya sidiri huku ukiupuchua kwa mikono huo mchanganyiko wako wa dawa mpaka uhakikishe mchanganyiko wako wote uwe umeenea mafuta ya sidiri. Zingatia kuwa mchanganyiko wako inatakiwa uwe umeenea mafuta ya sidiri lakini uwe katika hali ya ukavu (vumbi)

Uweke mchanganyiko wako huo katika  chupa ndogo ya kioo, funga mdomo wa chupa kisha livishe chupa lako kitambaa chenye rangi ya weusi au rangi nyekundu. Kalichimbie chupa lako na ulifukie sehemu ambayo kiasili hua haiyoti mimea au jaani (jalala la taka) au chini ya jiko la mafiga ya kuni, wakati wa usiku, liache hapo kwa muda wa siku saba kisha ulitoe na ulivue kitambaa, muda wa kulitoa ni lazima iwe mchana wakati jua lipo katikati ya dunia

Tumia dawa yako hiyo kwa kuirashia takita droo yako ya hela au sehemu unayo weka hela fanya zoezi hilo kila baada ya siku 7. Itunze dawa yako katiaka sehemu nzuri, epuka sehemu ambayo mwanamke anaweza akaishika akiwa katika hali ya hedhi.

Dawa hii inanguvu za ajabu za kuzuiya aina zote za chuma ulete.

Tafadhali usisome kisha ukaondoka bila ya kuacha maoni yako  au ushauri. Mualike na mwenzio ajitibu kipitia blog hii.

Thursday, January 30, 2014

DAWA YA MAPENZI


bwawa la wanga; dawa ya mapenzi kwa mwanamke au mwanaume anaekusumbua chukua jani la mti wa mkungu jani hili liwe la kwanza juu katika tawi la ncha ya mti huo. jani hilo huchumwa siku ya ijumaa kabla ya watu kusali au usiku wa siku ya jumanne

Piga hodi mara tatu katika mti huo hatua chache kabla haujafika ukiwa unaurushia unga wa dona ukikosa dona urushie sembe, utasema hivi -hood wakazi wa mti huu mimi nimekuja  kwenu kuchukua dawa itakayonisaidia katika shida yangu fulani (itaje) wala sikuja kwenu kuchukua sumu ya kumdhuru  mtu

zunguka mti huo mara moja kulia kwenda kushoto. Panda na uchume jani shuka nalo bila kuliangusha chini ukiliangusha jani hili hautoweza kufanikiwa jambo lako

likaushe juani kisha litwange na liwe unga laini. changanya unga huo na chumvi ya mawe  kisha utakua unachoma mchanganyiko huo katika kitezo hali ya kua unajifukiza ukiwa mtupu (uchi)

Siku ya kwanza kuchoma iwe ni siku ya ijumaa baada ya watu kumaliza kusali au usiku wa siku ya jumanne utaendelea kwa muda wa waku 14 mpaka 21. utakua unatia nia ya kumwita kimapenzi unaemkusudia.

Hakika atakujilia huyo ulie mkusudia hali ya kua ni mwenye bahaba makubwa kwako, mwambie jambo lako lolote atakubali na hato kupinga wewe kwa lolote. Usijaribu tumia njia hii na njoo hapa unicheki kwa matokeo mazuri

Mualike mwenzio ajitibu na kutatua mambo yake kupitia blog hii bwawalawanga.blospot.com 

TIBA YA UGONJWA WA SUKARI

bwawa la wanga. tiba ugonjwa wa sukari; unga wa shairi gram 100 unga wa ngano gram 100 habati soda gram 100. gundi (inafanana na ubani lakini haina harufu)

Chemsha dawa hizo katiaka vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika 10 zima moto acha ipoe. chuja weka katika chupa safi

matumizi kikombe kidogo asubuhi kabla ya kula chochote kwa muda wa siku saba. Wiki ya pili kunywa siku moja na uache siku moja

kwa muda wa wiki mbili utakua umepona na utaweza kula vyakula vyote ambavyo ulikua umekatazwa Inshallah

Miti hii saba ikichemshwa na kunywewa asubuhi kabla ya kula chochote kiasi cha nusu ya kikombe kidogo cha chai huponyesha maradh ya sukari.

Aloe vera (mshubiri)
Tango chungu
Mdalasini
Majani ya tini
Uwatu
Mbegu za zabibu
Habati soda.

Mualike mwenzio ajitibu kupita blog hii bwawalawanga.blogspot.com

DAWA YA UGONJWA WA SUKARI

bwawalawanga; tafuta dawa zifuatazo kwa ugonjwa wa sukari
Ubani makka gram 100
Shubiri gram 100
Mvuje gram 100
Habbat sowda gram 100

zisage dawa hizo na ziwe unga laini kisha zigawanye katika mafungu matatu sawa . changanya fungu moja na maji kiasi cha chupa mbili na uchemshe kwa muda wa dakika kumi ipua na iyache ipoe kisha chuja na uweke katiaka chupa safi

Tumia kila siku kiasi cha kikombe cha kahawa asubuhi kabla ya kula kitu chochote kwa muda wa siku 13. Ikiisha dawa hii chukua fungu la pili na uchemshe kama ulivyofanya katika fungu la kwanza. Tumia dawa hii katika muda wa siku 13. Itakapokwisha  chukua fungu la mwisho lichemshe kama ulivyofanya katika mafungu yaliyotangulia. Dawa utatumia kwa muda wa siku 14 hii itafanya siku za dawa kua 40

Baada ya siku hizo tatizo lako litakua limekwisha kwa idhni ya Allah na utaweza kula vyakula vyako vyote, hapo utakua umepona . Tumia halafu rudi hapa kwa dawa na tiba zingine. mualike mwenzio BWAWALAWANGA.BLOGSPOT.COM

DAWA YA KUNG'ARISHA USO KWA KUREMBESHA

 Rembesha uso kwa dawa hii ya asili; kanda unga wa habati soda katika mafuta ya zaituni utajipaka usoni  halafu upigwe na mwanga wa jua kidogo kisha osha kwa maji vugu vugu

rudi hapa kwa matokeo mazuri

DAWA YA KUZUIYA KUNYONYOKA NYWELE

Utakanda unga wa habati soda katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi changanya na mafuta ya zaituni kikombe kimoja

tumia dawa yako hiyo kwa kusugua kichwa kila siku jioni. osha kichwa kwa maji safi na sabuni
tumia dawa hiyo halafu njoo hapa unicheki kwa matokeo mazuri

DAWA YA KULAINISHA NGOZI

Tumia dawa hizi ili kulainisha ngozi
kama unangozi kavu changanya asali safi na robo kijiko cha habati soda

tumia dawa yako hiyo kwa kunywa kila siku asubuhi kabla ya kula chochote. dumu kutumia dawa hiyo kwa muda wa siku 30 mpaka 40 halafu njoo hapa unipe matokeo.

DAWA YA KUONDOA MABAKA MWILINI

Tumia dawa hizi kuondoa mabaka mwilini
Chukua vijiko vitatu vya unga wa habati soda uliosagwa  changanya na  siki inayotokana na juisi ya kitunguu saumu koroga ili upate mchanganyiko kisha weka vijiko vitano vya mafuta ya habati soda katika huo mchanganyiko wako

tumia kila siku kwa kupaka sehemu husika hali ya kua kama unasugua katiaka baka. endelea mpaka mabaka yatakapoisha. dawa hii huchukua muda wa siku kumi na nne mpaka ishirini na moja  kuondoa mabaka mwilini

Tumia dawa hiyo halafu njoo hapa unicheki kwa matokeo

DAWA YA CHUNUSI NA VIPELE


 Tumia dawa zifuatazo ili kuondoa chunusi na vipele mwilini;
chukua kikombe cha habati soda iliyosagwa. chukua nusu kikombe cha unga wa maganda ya komamanga changanya na siki inayotokana na juisi ya tufaha (apple)

paka sehemu inayotakiwa kila siku kabla ya kwenda kulala mpaka vipele na chunusi vitakapondoka. utunze mchanganyiko wako wa dawa sehemu baridi, mchanganyiko huo unaweza kukaa mpaka wiki tatu;

Dawa hii huondoa haraka vipele na chunusi  kama utatumia bila kukatisha. tumia dawa hiyo halafu njoo hapa unicheki kwa matokeo.